Mon, 06 February 2012

DON BOSCO YOUTH CENTRE UPANGA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MATARAJIO
Tupo katika hatua za mwanzo kuunda vikundi vipya kadiri ya mahitaji ya vijana:

  • Media club
  • Youth Rights Club
  • Environmental club etc.
  • Youth Centre Animators

Mlezi wa shughuli za vijana kituoni ni Pd. Bonifas Mchami.

DBYES – TANZANIA & UTUME KWA VIJANA
Don Bosco Youth Educational Services -TZ ni idara inafanya utume wa kuziunganisha na kuzijengea uwezo taasisi nyingine za Don Bosco kwa njia ya programu mbalimbali. Pia inatoa huduma katika majimbo mbalimbali Tanzania kwa kuwajengea uwezo walezi wa vijana. Baadhi ya programu maarufu za DBYES ni:
Chuo cha Maisha. Programu hii inaendeshwa katika parokia za Jimbo Kuu la Dar es salaam. Walezi wa vijana katika majimbo mengine zaidi ya kumi wamepewa mafunzo ya namna ya kutumia programu hii. Programu hii pia inapatikana kwa lugha ya kingereza. Mswada wenyewe unaitwa “Scaffoldings” Kimechapishwa na Pauline-Nairobi.
Uhai Tele – Radio programu. Vipindi hamsini vimerekodiwa na vinarushwa katika baadhi ya redio Tanzania. CD pia zinapatikana.
Vijana Publication – Hii ni huduma kwa njia ya uchapishaji. Kupitia huduma hii DBYES inawachochea vijana kukuza vipaji vyao vya kitaaluma. Tayari uchapishaji wa kitabu kimoja kimefanyika. “Mission One” mwandishi ni kijana tu – Erick Vedasto.
Uhamasishaji wa Miito: Idara hii pia inashughulika na uhamasishaji wa miito.  Nyenzo zinazotumika kwa mawasiliano ni: Vipeperushi, mabango maalumu, Vitabu, camp za miito, tamasha la miito n. k. Pia kila nyumba ya Don Bosco inaalikwa kuwa mhamasishaji wa Miito.  
Mkurugenzi wa DBYES-TZ na UTUME KWA VIJANA ni Pd. Augustine Sellam

MAFANIKIO

  • Elimu ya Dini mashuleni(CRE) inaendelea kupitia vipindi vya dini. Wanafunzi wengi wanapokea sakramenti mbalimbali: Ubatizo, Komunyo na Kipaimara.
  • Programu ya Chuo cha Maisha (Scaffolding) imeweza kuenea katika parokia 20 za Jimbo kuu la Dar es Salaam.
  • Elimu juu ya kujikinga na VVU/UKIMWI kupitia programu ya “Life Choices”
  • Album ya nyimbo za dini ya waimbaji wa “Holy Family Gospel Singers”. ipo madukani.
  • Katekesi na Ibada ya misa za vijana kila mwezi.
  • Tamasha la wazazi na wanafunzi wa YCS. Zaidi ya wanafunzi 2000 walishiriki.
  • Savio Basketball club daima kuwa kati ya tatu bora katika fainali zote za mchezo wa kikapu-Taifa. 
  • Karate Club kuweza kundaa maonyesho ya wazi kwa watoto na Vijana.

UONGOZI WA KITUO KWA SASA:
Pd. Fredrick Swai – Gombera (Rector)
Pd. Bonifasi Mchami – Administrator
Pd. Augustine Sellam – Prov Del. YM

WAHUDUMU WENGINE
Merry Urio – Secretary
Salome – Mpishi
Mama Diana - Mpishi
Leoni – Mazingira
Masai - Mlinzi
Neema Mtui – Mkufunzi (LC)
Alexander Mndanga – Mkufunzi (LC)
Das – Kocha (Kikapu) na Dereva
Prosper Dionis – SYM (TZ)

SHUKRANI
Kwa niaba ya uongozi wa kituo cha vijana DB-Upanga, tunapenda kuwashukuru wahudumu wote kwa moyo wao wa kujitolea daima katika kufanikisha malengo ya kituo. Pia viongozi wa vikundi vyote pamoja na vijana wote kwa ujumla kwa kuendelea kufika, kupanga na kutekeleza program zinazoandaliwa na kituo. Mwisho shirika la Don Bosco katika ngazi zote, Jimbo kuu la Dar es Salaam na wadau wote kwa msaada wa hali na mali. Mungu awabariki.

Imeandaliwa na: 
Prosper Kadogo
SYM-Coordinator - TZ

1 | 2